
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya kikao maalum na ujumbe wa wataalamu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, kwa lengo la kujadili masuala ya kisera na kiutendaji yanayohusu maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

Kikao hicho, kilichofanyika leo Aprili 30, 2026 jijini Dodoma, kilijikita katika kuchambua kwa kina fursa zilizopo, changamoto zinazoikabili sekta ya elimu, pamoja na kubaini mbinu bora za kuzitatua, ili kuboresha utoaji wa elimu na kuhakikisha unaendana na mahitaji ya maendeleo ya taifa.

Kwa upande wa Wizara ya Elimu, kikao kiliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Ibrahimu Liguo, aliyemwakilisha Katibu Mkuu, Prof. Carolyne I. Nombo. Kwa upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ujumbe uliongozwa na Linda Spahia, Mchumi Mwandamizi (Senior Economist).


