PROF. NOMBO ATAKA KASI NA UFANISI UTEKELEZAJI MRADI WA HEET.

 

Taasisi zinazotekeleza Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) zimetakiwa kuongeza kasi ya utekelezaji ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya na mageuzi makubwa ya kiuchumi kwa jamii na nchi. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiongoza kikao cha 4 cha Kamati ya Kitaifa ya uendeshaji wa Mradi kilichofanyika Jijini Dodoma Julai 09, 2024.

 

" Ni matarajio yangu kuwa kasi ya ufuatiliaji pia itaongezeka na leo tunaunda timu ndogo ya wanakamati 4 miongoni mwa wajumbe wa kamati ya uendeshaji na usimamizi wa mradi itakayofuatilia Taasisi zilizonyuma katika utekelezaji,"amesema Prof Nombo. Mradi wa HEET wenye thamani ya Dola Milioni 425 unatekelezwa katika Vyuo 22. Baadhi ya vyuo n taasisi wanufaika wa mradi ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo kikuu cha Dodoma, Chuo cha Ushirika Moshi, Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu Ardhi, Chuo cha Uhasibu Arusha na Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na tmTeknolojia, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na COSTECH.

Vyuo vingine ni MUHAS, Mzumbe, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Chuo kikuu cha Taifa zanzibar , IFM , Chuo cha Mipango na Chuo cha Takwimu Katika kikao hicho Bajeti ya mradi kwa mwaka wa fedha 2024/25 iliwasilishwa ambapo Shilingi Bilioni 457.6 zimeidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji ambapo 81% ya fedha hizo zitatumika katika shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu anuwai. Aidha kiasi kilichosalia kimeelekezwa katika kuwezesha matumizi ya TEHAMA, uboreshaji wa mitaala na uendelezaji wa watumishi.