
Wakati Wiki ya Kujifunza Kidijitali (Digital Learning Week) 2025 ikiingia siku ya pili Septemba 03, 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo ameshiriki mijadala ya kimataifa kuhusu mustakabali wa elimu barani Afrika.
Miongoni mwa mada alizoshiriki Katibu Mkuu huyo ni “New worlds of learning: How AI is reshaping the learning futures of students” na “Harnessing AI for the future of Education in Africa: Deepening divides or Bridging gaps”, ambapo alichangia hoja kuhusu nafasi ya teknolojia ya akili bandia (AI) katika kuleta usawa wa fursa za elimu na kuimarisha ubora wa ujifunzaji kwa vijana wa Afrika.
Viongozi wengine walioungana na Katibu Mkuu katika kongamano hilo ni pamoja na Amos Tengu, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Bi. Sekela Mwambegele, Afisa Mambo ya Nje.