Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa ufadhili wa masomo katika elimu ya juu kupitia Samia Skilashipu, na mwaka huu imeanzisha Samia Scholarship Extended AI/DS

kwa ajili ya wanafunzi wa Shahada ya kwanza katika fani za data science, artificial intelligence, cyber security, machine learning na allied science



Hayo yameelezwa Agosti 13, 2025 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mhe. Nicola Brennan, ambapo amesema kuwa mpango huo utawapa fursa wanufaika kusoma katika Vyuo Vikuu bora Duniani na kwamba Serikali imetenga Sh. Bilioni 5 kwa ajili ya utekelezaji.



Mhe. Brennan ameipongeza hatua hiyo ya kimkakati, na kwamba Serikali ya nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania kuongeza fursa zaidi za masomo kwa vijana wa Kitanzania kupitia Irish Fellowship Program na program mbalimbali, ikiwa na pamoja na kuunganisha vijana na makampuni mbalimbali ili kuwezesha mafunzo kwa vitendo.