Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amesema serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu hasa katika Ujenzi wa miundombinu na kutoa mafunzo Kwa Walimu kazini.



Amesema hayo Machi 7, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo ameongeza kuwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mbali ya uwekezaji huo imefanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kuja na Toleo la 2023



"Ndani ya miaka miwili tuliweza kufanya majadiliano na jamii ya Kitanzania kuweza kupata maoni na mahitaji ya Watanzania namna gani wanataka elimu yao iwe" amesema Nombo.



Kiongozi huyo amesema pamoja na kwamba zimetumia mbinu mbalimbali za kuelimisha umma wa Watanzania lakini bado wizara iliona umuhimu kukutana na kujadiliana na wahariri ili wapate uelewa wa mabadiliko yaliyofanyika ili waweze saidia katika kuwafikia Watanzania wengi zaidi.