Wadau mbalimbali wa Elimu leo Agosti 25, 2025 jijini Dar es Salaam wameshiriki katika Kongamano la Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kusherekea mafanikio ya taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake.



Kongamano hilo linahususha maonesho ya bidhaa za wanakisomo wa Taasisi hiyo zilizotokana na mafunzo ya vitendo na ubunifu wa washiriki.



Aidha, wanafunzi wa Taasisi wameandaa vifaa vya kujifunzia vinavyoakisi mbinu bunifu na shirikishi za elimu ya watu wazima.



Taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo endelevu nchini, ikiwemo vyuo vya ufundi, mashirika ya kijamii, na wadau wa maendeleo, zimeshiriki Kongamano hilo kuonesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kuendeleza elimu jumuishi na inayolenga matokeo chanya kwa jamii.



Kauli mbiu ya Kongamano hili ni Elimu bila Ukomo kwa Maendeleo Endelevu