Wizara ya Elimu ilianzisha Sheria ya Elimu mwaka 1962 kuashiria kuanza kwa mageuzi katika sekta ya elimu ambapo mkazo mkubwa uliwekwa katika kuwaandaa Watanzania kitaaluma ili kujaza nafasi za Serikali zilizokuwa zimechukuliwa na baadaye kuachwa wazi na wageni.
Hivyo, sheria ya elimu iliagiza shule zote za msingi kuongeza muda wa programu zao za masomo hadi kufikia miaka minane na kusisitiza umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa fursa za elimu ya sekondari.