
washiriki 50 wa Kambi Maalum ya Maarifa wamewasili rasmi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)
Kambi hii ya miezi 10, chini ya ufadhili wa SAMIA SCHOLARSHIP EXTENDED for DS/AI+, inalenga kuwaandaa vijana kujiunga na vyuo vikuu bora duniani. Inashughulikia Sayansi ya Data, Akili Unde, na Sayansi Shirikishi, na kuimarisha ujuzi wa kisayansi na teknolojia kwa vijana.
Washiriki wamewasili kikamilifu, huku mafunzo rasmi yakianza kesho, Septemba 15, 2025.
Kambi itajumuisha mafunzo, semina, na miradi ya vitendo, ikilenga kukuza vipaji na kuendeleza ujuzi unaohitajika kwa elimu ya juu na teknolojia.
Hii ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha elimu, utafiti, na ubunifu vinawafikia vijana na jamii.