Ubalozi wa Uingereza Nchini umejipanga kuimarisha mfumo wa utekelezaji miradi wanayofadhili katika sekta ya Elimu nchini ili iendani na Mageuzi ya Elimu nchini.



Hayo yamesemwa na Naibu Balozi na Mkurugenzi wa Maendeleo- Ubalozi wa Uingereza Nchini Bibi Kemmy Williams ambae amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Jijini Dodoma.



Katika Kikao hicho Profesa Mkenda ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kufadhili miradi katika sekta ya Elimu na pia amewapitisha katika mpango wa utekelezaji Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya Elimu.



Mkenda amesisiitiza juu ya kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji miradi kwa kuhakikisha miradi hiyo wanayofadhili inabuniwa kwa pamoja na inalenga kutekeleza mageuzi ya elimu ili kuleta tija na kuchangia kuongeza fursa za elimu, kupunguza changamoto zilizopo na kuwezesha kuandaa vijana wenye ujuzi na umahiri.



kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Katimu Mkuu Elimu Dkt Franklin Rwezimula, Kamishna wa Elimu Nchini Dkt Lyabwene Mtahabwa, Mkurugenzi wa Mipango Atupele Mwambene na Viongozi wengine kutoka kutoka Ubalozi wa Uingereza Bi Gertrude Mapunda - Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Watu na Bw. Colin Bangay- Mshauri wa Elimu.