Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria

  • Kutoa huduma na msaada wa kisheria kwa Idara na Vitengo vya Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara juu ya tafsiri ya sheria, masharti ya mkataba, masharti ya makubaliano, mikataba ya ubinafsishaji, mikataba ya manunuzi, dhamana, mikataba ya ushauri na aina nyingine ya makubaliano pamoja na nyaraka nyingine za kisheria;
  • Kutoa msaada wa kitaalamu katika maandalizi ya nyaraka za kisheria ikiwa ni pamoja na kutungwa kwa Sheria za Bunge na sheria ndogo na kuziwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
  • Kutoa huduma za kisheria kwa Wizara na Taasisi zake;
  • Kushiriki katika majadiliano na mikutano mbalimbali inayohusiana na utaalamu wa kisheria katika sekta za elimu,sayansi na teknolojia;
  • Kushirikiana na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika kufuatilia na kuhudhuria kesi za madai, jinai na madai mengine yanayohusu Wizara; na
  • Kutoa msaada wa kitaalamu kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali juu ya mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria kama vile amri, notisi, vyeti, makubaliano na nyaraka za uhamishaji.