Mradi wa Kuimarisha na Kuboresha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) jnaoyekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na OR TAMISEMI umeongeza fursa za uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, kutokanaa na uboreshaji na ujenzi wa miundombinu mipya ya kujifunzia.



Mratibu wa BOOST mkoani humo, Bw. Leonard Msendo, amesema kabla ya kuanza utekelezaji wa BOOST uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali ulikuwa chini ya asilimia 95. Mwaka 2023 waliandikishwa 22,800 sawa na asilimia 97.3%, mwaka 2024 idadi iliongezeka hadi 24,365 (109%), na mwaka 2025 wanafunzi 20,554 waliandikishwa (108%).



Ameongeza kuwa, uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza katika mkoa huo umeonyesha mwenendo chanya, ambapo mwaka 2023 wanafunzi waliosajiliwa walikuwa 20,053 (87%), idadi ikapanda hadi 24,004 (102%) mwaka 2024, na mwaka 2025 wanafunzi 22,840 (100%)