Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir Machi 30, 2026 jijini Dodoma amewasili katika viwanja vya Ofisi za Wizara hiyo, kwa ajili ya kugawa Vifaa Vya Kijiditi vya Kufundishia na Kujifunzia katika Shule za Awali na Msingi na Shule za Sekondari nchini.



Hatua hii ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika sekta ya elimu na kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu.