Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi Julai 23, 2025 Jijini Dodoma ameridhishwa na ubora na mazingira ya jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia  katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.



Amesema hayo alipotembelea Wizara akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya wizara na taasisi mbalimbali.



Akikagua jengo hilo amesema amefuruhishwa kuwa wizara imeamia na kuwa mazingira yameweka katika ubora unaowezesha kuongeza ari katika utendaji wa watumishi huku akipongea hatua ya kuanza kwa kituo cha huduma kwa wateja cha kisasa katika jengo hilo jipya.



Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo amesema jengo hilo limefikia zaidi ya asilimia 95 na kwamba lime chukua watumishi zaidi ya 400.



" Idara na Vitengo vyote viko katika jengo hili hivyo huduma zinatolewa kwa ukamilifu toka juni 1, 2025. na kupitia kituo chetu tunatoa huduma kwa wadau kwa njia mbalimbali za kidigitali."