
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeshiriki zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza Januari 27, 2026 Jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa sekta ya elimu inaendelea kuunga mkono maono ya Rais hususan katika kuinua kiwango cha elimu na kulinda mazingira.

Prof. Nombo ameeleza kuwa kupanda miti ni mwendelezo wa utamaduni wa kuhamasisha wanafunzi na jamii kushiriki katika kulinda mazingira.

Aidha, amebainisha kuwa wizara imeweka miongozo inayowawezesha wanafunzi na vijana kushiriki kikamilifu katika kampeni za kitaifa za upandaji miti.

"Leo, sekta ya elimu imeungana na Watanzania wengine katika kampeni ya kitaifa ya upandaji miti, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais". Amesesema Katibu Mkuu

Prof. Nombo amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itaendelea kuunga mkono tarehe 27 ya Kijani Kwa kupanda miti Kila Mwaka


