
Leo tarehe 15 Februari 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewasili Mkoani Tanga, wilayani Mkinga ambako Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mkinga inajengwa ili kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi hiyo.

Ujenzi wa kampasi hiyo ni utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), mradi unaolenga kuboresha miundombinu ya Vyuo Vikuu na kuimarisha ubora wa elimu ya juu nchini.

Sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi, Waziri Mkuu pia ameshiriki katika zoezi la kupanda mti wa kumbukumbu, ishara ya kuunga mkono juhudi za kulinda mazingira na kuendeleza urithi wa kijani katika maeneo ya elimu


