Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Programu ya Kuboresha Kada ya Ualimu (GPE TSP) inalenga kuboresha ujifunzaji jumuishi unaomlenga mwanafunzi kwa kuzingatia mabadiliko ya mifumo iliyoboreshwa, mipango, usimamizi na usawa wa kijinsia katika Kada ya Ualimu.



Akizungumza Machi 13, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa Programu hiyo Prof. Nombo ameongeza kuwa program hiyo pia itaimarisha mazingira ya walimu katika dhana ya ufundishaji na Ujifunzaji pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa Walimu watakaofundisha Wanafunzi wenye mahitaji Maalum