
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Sh. Bilioni 27 milioni 472 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Kaimu Mkuu Mkoa Mhe. Dadi Kolimba amesema fedha hizo zimetumika kujenga takribani madarasa 329, matundu ya vyoo 1046, Nyumba za walimu 22 na mabweni 15 mbali na uwekezaji mkubwa wa ujenzi kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe.

Amesema fedha hizo zinazotokana na miradi ya elimu ambayo ni BOOST, SEQUIP, EP4R na wadau wa wengine wa maendeleo.


