Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika kukuza elimu jumuishi, mbadala na endelevu, hususan kwa wananchi waliokosa fursa ya elimu katika mfumo rasmi.



Prof. Mushi amesema hayo Disemba 17, 2025 jijini Dar es Salaam katika Mahafali ya 64 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), akisisitiza kuwa maendeleo ya taifa yanategemea uwezeshaji wa wananchi kielimu, kiujuzi na kiakili.



Prof. Mushi ameipongeza TEWW kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Programu ya Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA), pamoja na maboresho ya mitaala inayozingatia mafunzo ya amali, stadi za maisha, ujasiriamali na matumizi ya teknolojia.



Kwa upande wake, Mkuu wa TEWW, Prof. Philipo Sanga, amesema jumla ya wahitimu 2,223 kutoka kampasi za Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza wametunukiwa vyeti na tuzo mbalimbali na wako tayari kushiriki katika shughuli za kijamii na kiuchumi.