Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameongoza kikao kati ya Wataalamu kutoka UNICEF na Wizara kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji wa elimu nchini.



Kikao hicho ambacho kimefanyika Jijini Dodoma Februari 6, 2024 pamoja na mambo mengine kimejadili juu ya ufundishaji na ujifunzaji wa kijiditali, utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2024 Toleo la 2023 na rasilimali zilizopo kwa ajili ya utafiti, ufatiliaji na tathmini katika Sekta ya Elimu.



Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu huyo amesema kuwa Wizara ipo katika mchakato wa kuwa na mwongozo katika suala la kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kufundishia na kujifunzia ili kuwezesha utekelezaji wa mtaala ulioboreshwa.