WIZARA YA ELIMU ,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
ASEHEMU YA MAFUNZO YA UALIMU
- UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia sehemu yake ya mafunzo ya Ualimu inasimamia na kutoa mafunzo ya Ualimu kwa vyuo 35 vya Ualimu vya Seilikali na vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali. Aidha kwa upande wa vyuo vya Ualimu vya Serikali, Wizara inatoa kozi Za Astashada ya Ualimu elimu Awali na Msingi, Stashahada maalumu ya ualimu sayansi (miaka 3) na Stashahada ya ualimu sekondari (miaka 2).
- SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA
- NGAZI YA ASTASHAHADA
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III. Aidha, sifa za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari katika masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati (miaka 03) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha ufaulu wa kiwango cha “C” katika masomo matatu katika hayo, mawili yawe ni ya tahasusi za masomo ambayo mwombaji anaomba kusomea.
- NGAZI YA STASHAHADA
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari kidato cha I-IV.
- AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO HAYO
- MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA ASTASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI
Na. | AINA YA MAFUNZO | VYUO | MUDA WA MAFUNZO |
1 |
Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi | Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC Mpuguso TC, Singachini TC, Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC,Tabora TC, MonduliTC, Sumbawanga TC na Dakawa TC |
Miaka 2 |
Astashahada ya Ualimu Elimu Maalum | Patandi TC, Kabanga TC na Mpwapwa TC |
Miaka 2 | |
3 |
Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali | Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Sumbawanga TC, Tabora TC |
Miaka 2
|
4 |
Astashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo |
Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC, Tabora TC |
Miaka 2
|
5 | Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium) |
Dakawa TC, Marangu TC, Tabora TC
|
Miaka 2
|
- MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI MASOMO YA SAYANSI, BIASHARA NA HISABATI
1 |
Stashahada ya Ualimu Sayansi, Biashara na Hisabati |
Monduli TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC, Tabora TC Mandaka TC (kwa masomo ya Sayansi na Hisabati) na Sinyanga TC (kwa masomo ya Biashara) |
Miaka 3
|
- MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (ASTASHAHADA YA ELIMU MSINGI ELIMU MAALUMU)
Na. | AINA YA MAFUNZO | CHUO | MUDA WA MAFUNZO | |
---|---|---|---|---|
| 1 | Astashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi | Patandi TC | Miaka 2 |
- STASHAHADA YA UALIMU SEKONDARI (MIAKA 2)
1 | Stashahada ya Ualimu Sayansi na Hisabati | Monduli TC, Mandaka TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC, Mamire TC na Tabora TC |
Miaka 2
| |
2 |
Stashahada ya Sayansi ya Jamii , Biashara na Lugha | Bunda TC, Mtwara (K) TC, Marangu TC, Nachingwea TC, Shinyanga TC, Mandaka TC, Mpuguso TC, Dakawa TC, Butimba TC, Tabora TC, Morogoro TC, Tarime TC, Shinyanga TC,
|
Miaka 2
| |
3 | Stashahada ya Ualimu Michezo, Muziki, Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonesho | Butimba TC |
Miaka 2
| |
Stashahada ya Ualimu Michezo, | Butimba TC , Mtwara TC na Mpwapwa TC |
Miaka 2
| ||