Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa serikali inaendelea na jitihada za kuondoa changamoto ya mdondoko wa wanafunzi



Prof. Nombo amesema hayo Machi 15, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipotembelea Baraza hilo ambapo amesema sehemu ya jitihada hizo ni pamoja na ujenzi wa shule za kata ili kuwapunguzia wanafunzi kutembea mwendo mrefu.



Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mikakati hiyo pia inahushisha ujenzi wa mabweni katika shule, ujenzi wa shule salama pamoja na kuwa na sera ya kuwarudisha shuleni wanafunzi waliokatisha masomo yao kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za ujauzito.