
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewaagiza wamiliki wa shule nchini kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa watoto wote hasa wale wenye mahitaji maalum ili kuhakikisha makundi yote yanafikiwa.
Waziri Mkenda ameyabainisha hayo Jijini Mwanza akifungua mkutano wa Wanawake Wamiliki wa taasisi binafsi za elimu nchini kuanzia ngazi ya awali hadi vyuo vya kati na kuongeza kuwa jitihada zinazofanywa na Serikali zakuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na fursa ya elimu kwa ujumuishi hivyo, ni vyema sekta binafsi nao waongeze kasi yakuleta mageuzi ya elimu hayo.
Aidha ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa kuzingatia Sera ya Elimu iliyoboreshwa ili kuandaa wahitimu wahitimu wenye elimu ujuzi ma umahiri kwa ajili ya ajira na hata zile za kujiajiri wenyewe.
Katika hatua nyingine Prof. Mkenda amewahamasisha wamilii hao kuwekeza pia katika Shule za Sekondari Mkondo wa amali bila kusahau kuchagiza mafunzo na matumizi ya sayandi na teknolojia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashauri wamiliki wa shule binafsi na vyuo kuiunga mkono serikali kwa vitendo ili kuhakikisha taifa linazidi linapata maendeleo kupitia sekta ya Elimu Sayandi na Teknolojia