Na WyEST
Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayanai na Tenolojia amesdhughulikia Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Prof.Daniel Mushi amesema Washauri wa Wanafunzi katika Vyuo wana nafasi kubwa ya kusaidia wanafunI kufikia malengo yao kielimu.



Amesema hayo Septemba 26 akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 43 wa Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania 1984 ( TACOGA1984 ) uliofanyika Maruhubi Kampasi ya Chuo Kikuu SUZA.



Amewataka washauri hao kuwa karibu na Wanafunzi na kuhakikisha wanatoa huduma hiyo kwa weledi mkubwa.

Prof. Mushi amepongeza Chama hicho kwa kuwa na programu za kuongeza ujuzi, ujenga uwezo na kuimarisha taaluma za utoaji huduma za ushauri nasihi na malezi hasa ukizingatia mabadiliko makubwa ya kiteknolojia katika wakati wa sasa.



TACOGA1984 inaundwa na Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania kinaundwa na wakurugenzi wa huduma za wanafunzi, maafisa wa ustawi wa wanafunzi , waratibu wa malezi na ushauri , wasimamizi wa mabweni pamoja na watumishi wote wanaohusika na masuala ya ustawi wa wanafunzi.