Wito huo umetolewa Machi 25, 2024 Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe akifungua Mdahalo wa nane wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya nchi za Afrika Mashariki unaofanyika katika Chuo Kikuu Ardhi Kampasi Kuu, mada kuu ya mdahalo ikiwa utangamano, amani na demokrasia katika nchi katika nchi hizo.



Mdoe amesema katika sensa ya watu na makazi zilizofanyika katika nchi wanachama zinaonyesha 70% ya wananchi ni vijana na watoto hivyo ni wajibu kuhakikisha ushiriki wa vijana katika shughuli zote za maendeleo ikiwemo uongozi na siasa.



Naibu Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa vijana wamekuwa na kawaida ya kuongea katika ya mitandao na midahalo ya kijamii, hivyo amewataka kushiriki katika michakato ya kisiasa na uchaguzi pamoja na kutoa hamasa na elimu juu ya demokrasia.



Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa amesema kuwa mdahalo huo unafanyika ikiwa ni sehemu ya kuwaandaa vijana ambao watakuwa viongozi wa kesho, hivyo jumuia hiyo imeamua kuwapatia majukwaa ya kukutana pamoja na kujadili juu demokrasia Amani na utangamano katika Jumuiya.



Kwa upande wake Afisa Mwandamizi Masuala ya Siasa kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki David Onen amesema Mdahalo huo unashirikisha nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki zote isipokuwa Somalia ambao imejiunga hivi karibuni na kuwa utachukua siku mbili.



Aidha amesema wajumbe watatoka na makubaliano ya namna ambavyo vijana wanaweza kushiriki katika kutunza amani na kuhamasisha demokrasia katika nchi zao huku maoni yao yakiwa chachu ya uboreshaji wa sera na miongozo mbalimbali ya kitaifa.