Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema kuwa Kongamano la Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima limeandaliwa kwa lengo la kufanya tathmini ya mafanikio, changamoto na mwelekeo wa baadaye wa elimu ya watu wazima nchini.



Akizungumza katika kongamano hilo, Prof. Nombo ameeleza kuwa ni fursa muhimu kwa wadau wa elimu kujadili kwa kina namna ya kuimarisha upatikanaji wa elimu jumuishi kwa makundi yote ya jamii.



Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 50, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima imekuwa na mchango mkubwa katika kuwajengea wananchi maarifa ya msingi, ikiwemo kusoma, kuandika na kuhesabu, sambamba na kuwapatia ujuzi.