Wadau wa Sekta ya Elimu kutoka makundi ya sekta ya umma, wawekezaji binafsi katika elimu, washirika wa maendeleo, na mashirika yasiyo ya kiserikali wamekutana jijini Dodoma 5 Septemba 2025.



Akifungua kikao hicho, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi amesema utekelezaji wa mpango huo wa tathmini za pamoja ni muhimu ili kuwezesha mipango ya pamoja ya maendeleo ya elimu nchini hasa katika kipindi hiki ambacho wadau wanatekeleza mageuzi ya elimu yanayolenga kutoa elimu ya ujuzi.



Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya ushirikiano (Annual Joint Education Sector Review) kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambavyo hulenga kufanya tathmini ya pamoja ya maendeleo ya sekta.