Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Prof. Maulilio Kipanyula, amesema kuwa mpaka sasa taasisi hiyo imewawezesha vijana kupata udahili katika vyuo mbalimbali duniani.



Ameeleza kuwa wanafunzi 16 wamepata nafasi nchini Afrika Kusini, 29 wamepata nafasi nchini Ireland, na watano wako katika hatua ya mahojiano ya ana kwa ana kwa ajili ya kupata udahili.



Katika hatua ingine , Prof. Kipanyula ameeleza kuwa taasisi hiyo inaendelea na ujenzi wa hosteli maalumu za wanafunzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 600 hadi kufikia 1000 ambapo wanaoishi katika hosteli wakitarajiwa kuongezeka kutoka 279 hadi 779.