
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, Agosti 15, 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na menejimenti ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (Open University of Tanzania - OUT) jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Prof. Mushi alipokea taarifa kuhusu hali ya utoaji elimu chuoni hapo pamoja na maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwatambua na kufahamiana na watumishi wapya wa menejimenti waliojiunga na chuo hicho.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili njia za kuboresha utoaji wa elimu na kuimarisha utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha chuo kinaendelea kutoa huduma bora na zenye tija kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.