Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo, wamepokea tuzo maalum kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima zilizotolewa kama ishara ya kutambua mchango wao mkubwa katika kusimamia na kuendeleza Elimu ya Watu Wazima nchini, hususan kwa juhudi zao za kuimarisha sera, mipango na utekelezaji wa programu zinazolenga kuwajengea uwezo wananchi wa rika mbalimbali.



Kupitia uongozi wao thabiti, Wizara imefanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya elimu ya watu wazima, ikiwemo kuboresha miundombinu ya kujifunzia, kuongeza ushiriki wa jamii, na kuhimiza ujumuishaji wa makundi maalum