Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo 2023 inahimiza matumizi ya TEHAMA, Teknolojia na Mifumo mbalimbali ya kibunifu katika Ufundishaji na Ujifunzaji kwa ngazi mbalimbali za Elimu.Ili Kufikia azma hiyo Tanzania inashirikiana na nchi mbalimbali na kubadilishana uzoefu katika eneo hilo ikiwemo nchi ya Brazil.Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Viongozi wengine wa Wizara na Taasisi wako nchini humo kwa ziara ya mafunzo na kupata uzoefu katika Taasisi ya Positivo iliyobobea katika teknolojia wezeshi za Elimu (EduTech). Uzoefu huo utawezesha utekelezaji wa Sera na mitaala mipya katika somo la TEHAMA ambalo litafundishwa kuanzia Elimu ya Msingi na pia kuja na Teknolojia mbalimbali za kuwezesha ufundishaji.Taasisi ya Positivo imefanya kazi na nchi nyingine barani Afrika ikiwemo Rwanda, Ghana, na Kenya ya kuandaa Mifumo ya Kitehama na teknolojia zinazowezesha na kurahisisha ufundishaji na ujifunzaji