
Naibu Katibu Mkuu wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hussein Omar, amesema changamoto kubwa kwa wahitimu wa Vyuo vya Ufundi (VETA) siyo mtaji pekee bali ni soko la bidhaa na huduma zao, hivyo suluhisho ni kuanzisha vikundi vya uzalishaji (clusters) vitakavyowawezesha vijana kujikusanyia mtaji na kupata masoko ya uhakika kupitia mfumo wa manunuzi ya Serikali.

Naibu Katibu Mkuu amesema hayo Januari 24, 2026 wilayani Chemba jijini Dodoma wakati ziara ya katika Chuo cha VETA Chemba ambapo amesema Serikali ndiyo mnunuzi mkubwa wa mahitaji kama sare za shule na viatu hivyo ni muhimu Kamati za elimu kwa kushirikiana na Wizara ya vijana na TAMISEMI kuhakikisha manunuzi hayo yanaelekezwa kwa vikundi vya wahitimu wa VETA.

Ameongeza kuwa hatua hiyo itawapa vijana soko la kudumu na kurahisisha upatikanaji wa mtaji kupitia fedha za asilimia 10 za Halmashauri, hivyo kuwasaidia kuondoka vyuoni wakiwa na ujuzi, vyeti na fursa za kujiajiri.


