Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Machi 14, 2024 jijini Dar es Salam amezindua Nyaraka za Usimamizi wa Maafa na kushuhudia zoezi la utayari wa kukabiliana na dharura za Kikemikali na Mionzi



Akizungumza kabla ya uzinduzi wa nyaraka hizo, Waziri Mkuu amezitaja kuwa ni pamoja na Mpango wa Kitaifa wa Maafa ya Kikemikali, Kibailojia, Kiradiojia na Nuklia na Mpango wa Kuitikia wakati wa dharura za Kinyuklia na Kiradiolojia ambayo imeandaliwa chini ua usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Nguvu za Atom Tanzania (TAEC).



Waziri Mkuu ameongeza kuwa kupitia nyaraka hizo Serikali imeweka mikakati ya pamoja ya namna ya kukabiliana na kujikinga na majanga yanayotokana na dharura za Kikemikali, Kibalojia, Kiradiolojia na Kinyuklia na kwamba zimezingatia masuala muhimu ya Kisera, uzoefu wa kukabiliana na majanga Kitaifa na Kimataifa.



Aidha, ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa Nyaraka za Usimamizi wa Maafa kwa wakati na kutoa mafunzo.



Waziri Mkuu pia ameagiza mazoezi ya utayari wa dharura za Kikemikali na Mionzi kuwa endelevu na kwamba Wizara zote na taasisi zinazohusika na utekelezaji wa nyaraka zilizozinduliwa kushiriki katika utekelezaji ili zisiwe nyaraka za makabatini tu