
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongeza mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu na diploma kutoka Shilingi Bilioni 460 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.2 ambayo ni makadirio ya mwaka wa fedha 2026/27

Akizungumza na Waandishi wa habari Januari 31, 2026 Jijini Dodoma Prof. Mkenda amesema kuwa sambamba na hilo, Serikali inakamilisha ujenzi kampasi mpya 16 za vyuo vikuu zinazojengwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kigoma, Lindi, Tanga na Tabora na kwamba uwekezaji huu unalenga kupanua fursa za elimu ya juu na kuhakikisha kila kijana anapata nafasi ya kusomea taaluma inayokidhi mahitaji ya soko la ajira.


