Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Februari 14, 2024 jijini Dodoma amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo katika Kikao Kazi cha mwaka kujadili masuala mbalimbali ya Wizara hiyo.



Awali katika salamu za Ufunguzi wa kikao kazi hicho Prof. Nombo ameeleza kuwa mafanikio yanayoonekana katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yametokana na juhudi za Watumishi wote ambao wamewajibika kikamilifu.



Amewataka kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara hususan utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mtaala Mipya ya Elimu