WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameshiriki kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Fedha Mhe Dkt Mwigulu Nchemba na Mawaziri wa Wizara mbalimbali leo jijini Dodoma.

Kikao hicho kililenga kujadili namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango na miradi yenye kutoa huduma kwa wananchi na maendeleo katika sekta mbalimbali.