Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wameipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, wakisema hatua hiyo imeimarisha mazingira ya kujifunza na kufundisha.



Hayo yameelezwa katika Mkutano Mkuu wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu uliofanyika Oktoba 24, 2025 jijini Dodoma, Mohammed Saidi kutoka Shule ya Msingi Dodoma, ambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum, amesisitiza umuhimu wa kuwajali wanafunzi kama yeye kwa kuwapatia vitabu, viti mwendo, walimu mahiri na kutambua vipaji vyao.



Nenelo Mdachi wa Shule ya Sekondari Viwandani na Zaituni Halfan wa Sekondari Nzuguni walihimiza kushughulikia changamoto za kimaadili miongoni mwa walimu. Wamesisitiza utekelezaji wa Mwongozo wa adhabu ili kuimarisha nidhamu, maadili na taaluma shuleni.



Mohamod Idi kutoka Sekondari Umonga alitoa wito wa kuongezwa kwa walimu wa Sayansi na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mkondo wa Amali. Alisema mkondo huo unasaidia kukuza maarifa ya vitendo na kuandaa wataalamu wa baadaye.