
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema serikali imeandaa mkakati wa Kisayansi wa kuboresha kitaifa wa kuimarisha umahiri katika kuandika, kusoma na kuhesabu ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za Mhe Rais kwa Watanzania.

Amesema mpango huo ni nyenzo ya kuimarika ujifunzanzaji na ufundishaji KKK ili kuondoa kabisa changamoto ya wanafunzi kufika Darasa la tatu wakiwa hawajui Kusoma, kuandika na kuhesabu.

Prof. Mkenda ameeleza maeneo makuu ya utekelezaji ni pamoja na kuimarisha njia za ufundishaji kupitia mafunzo endelevu kwa walimu, maandalizi ya vifaa shirikishi vya kufundishia, mapitio ya mitaala hususan masomo ya sayansi, tathmini ya mara kwa mara ya maendeleo ya wanafunzi, na ushirikishwaji wa jamii katika mchakato wa elimu.

Amesisitiza kuwa mpango huu utatekelezwa kwa miaka mitano hadi 2030, na kutakuwa na mrejesho wa kila mwaka kuonyesha hatua ilifikiwa kwa umahiri wa wanafunzi


