Zoezi la upandaji wa Miti 250 kiwilaya lililofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kigamboni, kata ya Somangila Wilayani humo.lengo la kupanda Miti katika eneo hilo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila Wilaya nchini Tanzania inapanda miti 1,500,000 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.