Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Viongozi mbalimbali Disemba 15, 2025 wamekagua maandalizi ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Kagera ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



Mgeni rasmi katika Hafla hiyo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.