IDARA YA UTHIBITI UBORA WA SHULE

 

  1. MUUNDO WA UONGOZI WA UTHIBITI UBORA WA SHULE

Idara inaongozwa na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora wa Shule akisaidiana na Wakurugenzi Wasaidizi  wa Uthibiti Ubora wa Shulewa vitengo vitatu (03), ambavyo ni Kitengo cha Msingi,Sekondari na Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.

  1. OFISI ZA UTHIBITI UBORA WA SHULE

Ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule zipo katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na katika Halmashauri 184.

 

  1. MAJUKUMU YA IDARA YA UTHIBITI UBORA WA SHULE
  1. Kufanya  shughuli za Uthibiti Ubora wa Shule wa nje ya shule (external school quality assurance) ili kuona kama utoaji wa elimu katika ngazi zote husika unazingatia Sera, Sheria, Kanuni, Viwango, Taratibu na Miongozo iliyowekwa;
  2. Kufanya tathmini maalum ya usajili na kupendekeza kuhusu kusajiliwa au kutosajiliwa kwa shule za Awali, Msingi, Sekondari na vyuo vya Ualimu;
  3. Kufanya tathmini maalum/uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazojitokeza katika taasisi za Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya FDC na kutoa ushauri wa utekelezaji kwa wahusika wakuu;
  4.  Kufuatilia na kutathmini ubora na utekelezaji wa mipango ya Uthibiti Ubora wa ndani  ya Shule katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Elimu Maalum, Elimu ya Watu Wazima  na Nje ya Mfumo rasmi, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya FDC;
  5. Kumshauri Kamishna wa Elimu katika masuala yanayohusiana na Uendeshaji na Usimamizi wa Shule katika ngazi ya  Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Elimu Maalum, Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo rasmi, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya FDC;
  6. Kuandaa na kuwasilisha taarifa mbalimbali za Idara kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na Katibu Mkuu.
  7. Kufanya tafiti tatuzi (action research) utakaosaidia kuboresha ufundishaji, usimamizi na uendeshaji wa Shule/Vyuo; na
  8. Kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani  Tanzania ili  kuhakikisha kunakuwepo na  Elimu inayozingatia viwango bora katika ngazi zote za ElimuMsingi.