Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa Serikali imejipanga kwa dhati kuimarisha elimu ya juu nchini.



Prof. Mushi ameeleza hayo leo hii Novemba 7,2025 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na viongozi mbalimbali kutoka Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu ya juu.



Mushi amesema baadhi ya hatua zinazochukuliwa kuwa ni pamoja na kuongeza nafasi za mafunzo ya uzamili na uzamivu kwa watumishi wa vyuo, kuimarisha motisha na masilahi, pamoja na kuimarisha tafiti na mazingira kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo.