Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imepongeza Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuwezesha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kujenga Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Ikungi kwa ubora.Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baada ya kukagua chuo hicho, leo, tarehe 28 Machi 2024, Wajumbe wa PAC wameridhishwa kwa kiasi kikubwa na Ubora wa Majengo na gharama za Ujenzi zilizotumika, huku wakirejea na kuzungumzia tofauti ya hali waliyoikuta katika maeneo mingine waliyotembelea.“Mmetutia Moyo, tumetoka na Moyo ulionyooka. Tulikuwa Tumesononeka sana baada ya kutembelea Miradi mingine iliyojengwa kwa utaratibu huu wa Force Account,” amesema Makamu Mwenyekiti wa PAC, Mheshimiwa Japhet Hasunga.kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu profesa Carolyne Nombo ameishukuru kamati ya (PAC) kwa ziara yao katika chuo cha VETA Ikungi nakusisitiza kuwa Wizara inaendelea kuhakikisha huduma yavElimu ya amali inaendelea kusogezwq karibu na wananchi katika Wilaya zote nchini.Nombo ameongeza kuwa Matumizi ya Nishati safi (nishati Jadidifu) yabazingatiwa na kwamba Wizara itahakikisha Vyuo vya VETA vinanyo endelea kujengwa wanatumia Nishati Safi." kwa upande wa Nishati safi tutahqkikisha vyuo vote vilivyo chini ya Wizara ikiwemo vya VETA vinatumia Nishati safi kama ambavyo Rais wetu ameagiza na kusisitiza" amesema NomboNaye Mbunge wa Katavi na mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ametumia muda mwingi kukagua majengo na miundombinu mbalimbali na kubaini kuwa kiwango cha ujenzi wa chuo hicho ni cha ubora wa hali ya juu.“Mheshimiwa Mwenyekiti (wa PAC), nimezunguka maeneo mengi, kwenye Karakana, Vyoo na Madarasa, kazi hii ni nzuri sana kwa force account, Hata majengo yamejengwa kwa spacing (kuacha nafasi), jambo ambalo linasaidia hata kupunguza madhara inapotokea majanga kama moto,” amesema.