Serikali inaendelea na uhamasishaji wa usomaji vitabu katika ngazi mbalimbali za elimu. Katika kutekeleza  hilo imejenga maktaba katika vyuo vya ualimu na kuziwekea vitabu na kompyuta.

Pichani Walimu tarajali wa Chuo cha Ualimu Korongwe  wakitumia Maktaba iliyojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP).

Maktaba hii yenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wanachuo 500 na yenye sehemu ya Maktba mtandao inayochukua wanachuo zaidi ya 50 mbali na kutumiwa na Jumuiya ya Chuo cha Ualimu Korongwe pia inatoa nafasi kwa wananchi wa Korogwe kuitumia ikiwemo wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari waliopo maeneo ya karibu na chuo hicho.