Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Husna Sekiboko, leo Machi 10, 2026 imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika mwaka wa fedha 2025/2026.



Taarifa hiyo imelenga kuonesha hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, pamoja na mafanikio, changamoto na mipango ya kuimarisha utoaji wa elimu bora nchini.