Na WyEST*
Mkinga, Mkoani Tanga

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafadh Ameir, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Daniel Mushi, leo Februari 14, 2026 wamewasili mkoani Tanga kukagua maandalizi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe.



Uwekaji wa jiwe la msingi utafanyika tarehe 15 Februari 2026 na Waziri Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ambapo hii inaashiria rasmi kwamba Wilaya ya Mkinga sasa inakwenda kuwa mwenyeji wa Kampasi ya Chuo Kikuu Mzumbe, hatua itakayoongeza fursa za upatikanaji elimu ya juu kwa vijana wa Tanga na mikoa mingine nchini.



Kampasi hii haitatoa tu mafunzo ya kitaaluma, bali pia inatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Mkinga na Mkoa wa Tanga kwa ujumla, kupitia ajira, huduma, na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi zitakazofanyika katika eneo hilo