Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kutekeleza ahadi za Mhe. Samia Suluhu Hassan la utoaji ufadhili wa masomo kwa wanasayansi kupitia "Samia Scholarship" ili kuongeza wigo wa wanasayansi nchini ikiwemo sayansi ya Data na Akili unde



Prof. Mkenda amesema kuwa katika eneo hilo vijana 50 wanaenda katika vyuo vikuu bora nje ya nchi. Kati yao vijana 16 wanaondoka tarehe 1 Februari kwenda Chuo Kikuu cha Johannesburg kusomea shahada ya kwanza katika sayansi ya data na akili unde na Vijana wengine 34 wanatarajiwa kwenda Ireland mwezi Machi.



Amesema vyuo wanavyo kwenda kusoma pamoja na kuwa kuwa vina mfumo mzuri wa kupeleka vijana katika makampuni makubwa katika nchi hizo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo