Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kutokana na Mageuzi ya Kisera mafunzo ya ualimu yataanza kutolewa katika ngazi ya Diploma, na kwamba ngazi ya Astashahada haitakuwepo tena.



Akizungumza Aprili 26, 2026, Mjini Morogoro wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi sa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Dakawa, Prof. Mkenda ameongeza kuwa sifa ya chini ya kujiunga na mafunzo hayo itakuwa ni kuanzia kidato cha sita na kuendelea.



Aidha, amesema kuwa katika kuhakikisha nchi inakuwa na walimu wa kutosha wa masomo ya amali baadhi ya Vyuo hivyo vitakuwa maalum kwa ajili ya kuwaandaa ualimu wa hao na kwamba Masomo ya biashara na ujasiriamali yatafundishwa katika Vyuo vyote.