
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack amesema Mkoa huo utakuwa kinara kwa vijana wengi wa Lindi kujiunga na kusoma katika Kampasi ya Lindi ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mhe. Telack amesema hayo Desemba 20, 2025 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Lindi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amebainisha kuwa Mkoa huo ni wa Sita Kitaifa katika ufaulu wa mitihani iliyopita wa kidato cha Sita ambapo kwa matokeo hayo vijana wote wanaomaliza kidato cha sita wanaweza kuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu.

Ameishukuru Serikali na Wizara ya Elimu kwa kuleta tabasamu kwa wananchi wa Mkoa huo, kwani kampasi hiyo itatoa majibu ya kuwezesha kilimo chenye tija na huduma za utafiti kwa maeneo mengine ya kimkakati.


