Kampasi ya Lindi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itajikita katika program za Kilimo, Sayansi ya Udongo, Teknolojia na Usindikaji wa Vyakula.



Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Lindi, Disemba 20, 2025 Makamu Mkuu wa UDSM Prof. William Anangisye amesema program nyingine ni Biashara za Kilimo, pamoja na maeneo shirikishi ikiwemo Madini, Mazingira na Ulinzi wa Mambo ya Kale.



Prof. Anangisye ameongeza kuwa Kampasi hiyo itachochea tafiti, zinazotoa suluhu ya changamoto katika jamii. Vilevile wanufaika watapata elimu ya juu inayozingatia mafunzo kwa vitendo.