Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mwaka ujao wa masomo 2026/27, utakaoanza Oktoba Kampasi ya UDSM Lindi itapokea wanafunzi wa kwanza.



Katika hafla ya uwekaji jiwe la Msingi la ujenzi wa Kampasi hiyo Disemba 20, 2025 mkoani Lindi Mhe. Kikwete amesisitiza kuwa Chuo hicho kinajivunia juhudi za Serikali katika ujenzi wa mindombinu kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).